Seti ya bure ya zana katika lugha tofauti ambazo zinafanya kazi bila data. Zana hizi za Hesperian zimefanyiwa majaribio na jamii mbalimbali, na hutoa kipaumbele kwanza juu ya faragha ya mtumiaji.
Seti ya bure ya zana katika lugha tofauti ambazo zinafanya kazi bila data. Zana hizi za Hesperian zimefanyiwa majaribio na jamii mbalimbali, na hutoa kipaumbele kwanza juu ya faragha ya mtumiaji.
Tunakuwa na afya bora zaidi tunapojiamulia lini kufanya ngono, lini kupata mimba, na lini kupata watoto. Zana za Hesperian katika lugha tofauti hutumika kwa vitendo na zimebeba taarifa na nyenzo za afya ya uzazi zinazoaminika. Baada ya kupakua, zana hizi hufanya kazi bila intaneti au data. Zitumie katika kufanya maamuzi ambayo yatahakikisha matokeo yenye afya zaidi kwako, wapendwa wako, na jamii yako.
Unaweza kuangalia Sera yetu ya Faragha ya Zana za Mtandaoni hapa (kwa Kiingereza)
Zana ya Utoaji Mimba Salama
Jipatie hatua kwa hatua taarifa sahihi na pana juu ya utoaji mimba salama. Linganisha njia salama tofauti za utoaji mimba, tumia kikokotoo cha wiki za mimba, na jibu maswali au tafakari changamoto za kawaida kwa kutumia nyenzo pana ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ). Ikidhamiriwa kutumiwa na watu binafsi, wafanyakazi wa afya, waelimishaji na watetezi, Zana ya Utoaji Mimba Salama ni ndogo kupakuwa(chini ya mb 40) na imebuniwa kuhakikisha faragha ya mtumiaji.
LAUGHA ZILIZOPO
Lugha zaZana ya Utoaji Mimba Salama:
- KiAfaan KiOromoo
- KiAmharic
- Kifaransa
- Kiganda
- Kihispania
- Kiigbo
- Kiingereza
- Kinyarwanda
- Kireno
- Kiswahili
- Kiyoruba
Badili kati ya lugha 11 zote wakati wowote
Zana ya Uzazi wa Mpango
Zana hii, ambayo ilitengenezwa kwa ajili ya wafanyakazi wa afya wa mstari wa mbele,viongozi wa jamii, na waelimishaji rika, imesheheni picha, vielelezo, na taarifa zinazoeleweka kwa urahisi, na nyenzo shirikishi kusaidia majadiliano juu ya afya ya uzazi. Zana ya Uzazi wa Mpango imebeba mada muhimu kwa ajili ya ushauri nasaha zikiwemo jinsi kila njia inavyotumika, ufanisi wake katika kuzuia mimba, urahisi katika kuitumia kwa faragha, na kero zake.
LAUGHA ZILIZOPO
Lugha za Zana ya Uzazi wa Mpango:
- KiAfaan KiOromoo
- KiAmharic
- Kifaransa
- Kiganda
- Kihispania
- Kiingereza
- Kinyarwanda
- Kireno
- Kiswahili
Badili kati ya lugha 11 zote wakati wowote
Zana ya Ujauzito na Kujifungua
Zana ya Ujauzito na Kujifungua Salama hutoa taarifa sahihi na zenye kueleweka kwa urahisi juu ya ujauzito,kujifungua na huduma baada ya kujifungua. Vielelezo na lugha rahisi huifanya zana hii kutumika kwa vitendo na kwa urahisi na wafanyakazi wa afya wa ngazi ya jamii,wakunga, na watu binafsi na familia zao. Zana hii haina gharama, ni nyepesi kupakua na hufanya kazi bila mtandao.
LAUGHA ZILIZOPO
• Kifaransa
• Kihispania
• Kiingereza
• Kiswahili
Badili kati ya lugha 4 zote wakati wowote.