Zana ya Utoaji Mimba Salama
Seti ya bure ya zana katika lugha tofauti ambazo zinafanya kazi bila data. Zana hizi za Hesperian zimefanyiwa majaribio na jamii mbalimbali, na hutoa kipaumbele kwanza juu ya faragha ya mtumiaji.
Jipatie taarifa sahihi, pana na rafiki kwa mtumiaji juu ya kusitisha ujauzito. Ikiwa imeandikwa katika lugha inayoeleweka kwa urahisi na isiyohukumu, zana ya Utoaji Mimba Salama inaweza pia kuwasaidia watu wanaohitaji au wanaotoa huduma baada ya mimba kutoka. Pakua zana hii bure au tumia zana kwenye tovuti yetu.
Lugha za Zana ya Utoaji Mimba Salama: KiAfaan KiOromoo, KiAmharic, Kifaransa, Kiganda, Kihispania, Kiigbo, Kiingereza, Kinyarwanda, Kireno, Kiswahili, na Kiyoruba. Badili kati ya lugha 11 zote wakati wowote.
Zana hii haikusanyi taarifa zozote binafsi!
Unaweza kuangalia Sera yetu ya Faragha ya Zana za Mtandaoni hapa. (kwa Kiingereza)
Lugha za Zana ya Utoaji Mimba Salama: KiAfaan KiOromoo, KiAmharic, Kifaransa, Kiganda, Kihispania, Kiigbo, Kiingereza, Kinyarwanda, Kireno, Kiswahili, na Kiyoruba. Badili kati ya lugha 11 zote wakati wowote.
Zana hii haikusanyi taarifa zozote binafsi!
Unaweza kuangalia Sera yetu ya Faragha ya Zana za Mtandaoni hapa. (kwa Kiingereza)
Tazama video na kupakua programu!
Tumia Zana kwenye Mtandao
Tumia Zana katika ukurasa huu kwenye kisakuzi chako (browser) bila kupakua
Ndani ya Zana ya Utoaji Mimba Salama
-
Utapata maelezo kamili na yanayoeleweka ya njia za utoaji mimba salama: utoaji mimba kwa vidonge, ufyonzaji(suction), na utanuzi wa via na uondoaji wa mimba(D& E).
-
Utapata taarifa juu ya dozi na njia sahihi za kutumia vidonge vya misoprosto( pamoja na au bila mifepristoni) kwa ajili ya utoaji mimba kwa dawa wa mimba zenye wiki tofauti
-
Utajifunza utarajie nini wakati na baada ya mimba kutoka, ikiwemo ufanye nini pale dalili za hatari zinapojitokeza
-
Utajiandaa na kupanga namna ya kusimamia kwa usalama zoezi la utoaji mimba kwa kutumia orodha ya mahitaji muhimu, na kupata mapendekezo juu ya namna ya kuuhudumia mwili na mawazo yako
-
Utachunguza “taarifa juu ya nchi yako” kupata mashirika ambayo yanaweza kusaidia pamoja na viunganishi kwa sheria na kanuni zinazohusika
-
Utajibu maswali na kutafakari changamoto za kawaida kwa kutumia sehemu pana ya FAQ
-
Utasikiliza taarifa kwa kutumia nyenzo ya kusoma kwa sauti unapotumia zana hii katika Kiingereza, Kihispania, Kireno au Kifaransa
Zana ya Utoaji Mimba Salama imebuniwa kuhakikisha faragha ya mtumiaji. Kama unapakua zana kwa ajili ya matumizi, inahitaji chini ya mb 40 na hufanya kazi kwa ukamilifu bila data baada ya hapo. Kwenye kifaa chako, jina linalosomeka chini ya alama za zana ni “SA” tu
Kiongozi cha Haraka cha Zana ya Utoaji Mimba Salama
Chapisha mwongozo
Maagizo ya mkusanyiko wa haraka
Bofya picha hapa chini ili kupanua.
Zana ya Utoaji Mimba Salama inaimarisha na kusaidia kazi za wanaharakati, mashirika na makundi mengine yanayopigania fursa ya watu wote duniani kupata huduma ya utoaji mimba salama
Tusaidie kuboresha Zana hii!
Tuambie namna ya kuboresha zana hii.
Tuma maoni yako kwa [email protected]