Ni bure • imefanyiwa majaribio na Jamii mbalimbali • Hufanya kazi bila intaneti •
Haikusanyi taarifa
Zana ya Ujauzito na Kujifungua Salama hutoa taarifa sahihi na zenye kueleweka kwa urahisi juu ya ujauzito,kujifungua na huduma baada ya kujifungua. Vielelezo na lugha rahisi huifanya zana hii kutumika kwa vitendo na kwa urahisi na wafanyakazi wa afya wa ngazi ya jamii,wakunga, na watu binafsi na familia zao. Zana hii katika lugha ya Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa na Kihispania ni ndogo, hupakuliwa bure na hufanya kazi bila intaneti.
Unaweza kuangalia Sera yetu ya Faragha ya Zana za Mtandaoni hapa (Kiingereza)
Zana ya Ujauzito na Kujifungua Salama inajumuisha:
-
Kubaki mwenye afya wakati wa ujauzito – jinsi ya kula vizuri, upime nini wakati wa ujauzito, jinsi ya kudhibiti kichefuchefu na matatizo ya kawaida
-
kufanya zoezi la kujifungua kuwa salama zaidi – mahitaji ambayo yanapaswa kuwa tayari kabla ya kujifungua, jinsi ya kusaidia katika kila hatua ya uchungu, kutambua dalili za hatari na pale huduma ya dharura inapohitajika
-
huduma baada ya kujifungua – jinsi ya kumhudumia mtoto na mama mara baada kujifungua, na katika wiki ya kwanza, ikijumuisha kumsaidia kukabiliana na msongo unaofuatia kijifungua (post-partum depression) na katika kunyonyesha
-
taarifa za namna ya kutenda – rejea ya haraka ya mbinu za huduma za kiafya kwa kila mada
-
Tumia Zana kwenye Mtandao
-
Tumia nyenzo ya kusoma kwa sauti kusikiliza maudhui ya sehemu yoyote ya zana hii.