Zana ya Uzazi wa Mpango
Seti ya bure ya zana katika lugha tofauti ambazo zinafanya kazi bila data. Zana hizi za Hesperian zimefanyiwa majaribio na jamii mbalimbali, na hutoa kipaumbele kwanza juu ya faragha ya mtumiaji.
Zana hii, ambayo ilitengenezwa kwa ajili ya wafanyakazi wa afya wa mstari wa mbele,viongozi wa jamii, na waelimishaji rika, imesheheni picha, vielelezo na taarifa zinazoeleweka kwa urahisi, na pia ina nyenzo shirikishi kusaidia majadiliano juu ya afya ya uzazi. Zana ya Uzazi wa Mpango imebeba mada muhimu kwa ajili ya ushauri nasaha zikiwemo jinsi kila njia inavyotumika, ufanisi wake katika kuzuia mimba, urahisi katika kuitumia kwa faragha, na kero zake.
Zana ya Uzazi wa Mpango imejumuisha:
-
njia za uzuiaji mimba – taarifa juu ya njia za vizuizi, tabia(njia za asili), homoni, na njia za kudumu-kila njia na ufanisi wake, faida na mapungufu yake
-
Nyenzo ya kusaidia kuchagua njia – nyenzo shirikishi ambayo huwasaidia watumiaji kutafuta njia za uzuiaji mimba ambazo zinakidhi zaidi upendeleo wao, mtindo wa maisha, na historia ya afya yao
-
FAQs – sehemu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara inatoa majibu kwa maswali mengi ya jumla juu ya uzuiaji mimba na changamoto za kawaida juu ya njia mahsusi kama vile iwapo unaweza kutumia kondomu moja zaidi ya mara moja, na lini unaweza kuanza kutumia kila njia baada ya kujifungua, mimba kuharibika, au kutoa mimba
-
vidokezo na mifano shirikishi ya ushauri nasaha – boresha stadi zako za ushauri nasaha, kujisikia vizuri katika kujadili taarifa za afya ya uzazi, na kuweza kuwasaidia watu kutoka asili na mazingira mbalimbali
Tumia Zana kwenye Mtandao!
Tusaidie kuboresha Zana hii!
Tuambie namna ya kuboresha zana hii.
Tuma maoni yako kwa [email protected]